zusammen gärtnern

Bustani ya kimataifa na kuhusika

Je unapenda kulima mboga mwenyewe? Je unapenda kufahamu watu wengine? Je unapenda kulima, kula na kusherekea pamoja na watu wengine?

Tangia mwezi wa sita 2016 pale kwa mto wa kijiji pempeni ya mtaa wa Vauban inatengenezwa bustani ya kimataifa na kuhusika. Kwa kuheshimiana tunapenda kufanya kazi kwa pamoja, kufundishana, kufaidi na kufurahi pamoja.

Siyo muhimu umetokea wapi, unaongea lugha gani, una umri gani, kama una tatatizo lolote au la au kama una uzoefu katika kilimo au la: Njoo ushirike katika bustani ya jamii pale karibu na mto.

Tutafurahi kukuona!

MIADI 2018
Siku za mazoezi
10.März, 14. April, 12. Mai, 9. Juni, 14. Juli, 8. September, 6. Oktober, 17. November
kila mara kuanzia saa nne asubuhi.

Usimamizi wa shamba ndogo
Kuanzia mwezi wa tatu 2017 kutakuwa na nafasi za kusimamia shamba ndogo ndogo katika bustani ya kimataifa na kuhusika „zusammen gärtnern“. Unakaribishwa sana kushiriki na kujiandikisha. Hapa kuna fomu yake.

Warsha/matukio
Zinatangazwa kwa njia ya newsletter (kwa kijerumani, kiingereza). Jiandikishe tafadhali:

Mawasiliano: garten@zlev.de

Na mahali tunapopatikana
Trein ya barabara namba 3 kuelekea „Vauban“, shuka „Innsbrucker Straße“, halafu fuata vibao.

 rudi